Sunday, December 27, 2009

KUBALI TATIZO LAKO ULITATUE

MPENZI msomaji, nakukaribisha tena katika safu hii ya Maisha Yetu. Leo tutaangalia njia mbalimbali za kukusaidia unapopatwa na matatizo.Mara nyingi mtu anapopatwa na matatizo hubabaika na kujikuta hana msaada wowote.Mtu huyo huwa anashindwa kujikubali kama yupo salama na lipo tumaini jipya baada ya matatizo hayo anayokabiliana nayo.Ni watu wachache wanaojikubali kuwa wana matatizo na kutafuta njia ya kukabiliana nayo.Wengi walio na misukosuko hukosa furaha na kujiona kuwa ni wanyonge, waliokataliwa na jamii inayowazunguka.Hali hiyo huwafanya afya zao kuzorota na kukabiliwa na magonjwa mbalimbali kama ya moyo na vidonda vya tumbo.Kutokana na hali hiyo inayomkabili mtu huyo, jamii, ndugu na hata marafiki zake huwa mbali naye na kuacha kutoa ushirikiano wa karibu kwake.Ni vizuri kuelewa kuwa,...

USIKUBALI KUKATISHWA TAMAA

MSOMAJI, katika mfululizo wa makala hizi za maisha yetu, nimedhamiria kukuletea kitu kipya kila Alhamisi. Leo tutaangalia jinsi ya kutokufuata mawazo ya wale wanaotaka kukurudisha nyuma kimaendeleo.Miongoni mwa jamii tunazoishi, huwa kuna baadhi ya watu ambao hufurahia wenzao wanaposhindwa kutimiza malengo waliojiwekea.Ama huwa na tabia ya kuwakatisha tamaa wanaopenda kujikwamua kutoka katika hatua moja na kuelekea hatua nyingine.Watu hao mara zote huwakatisha tamaa wenzao kwa jambo fulani, kwa kuwaambia kuwa, wasijaribu kulifanya kwa kuwa hawatafanikiwa.Kumbe watu hao, ilitakiwa kuwatia moyo wale wanaotaka kujikwamua kiuchumi kwa kuwaambia kuwa, wajaribu kufanya jambo walilolikusudia.“Mawazo ya watu kama hao wasiopenda mafanikio ya wengine mara zote ni sumu ya maendeleo”.Hivyo unapokutana...

IMANI HULETA MAFANIKIO

NAKUKARIBISHA, katika mfululizo wa makala hizi za maisha yetu, zinazokujia kila Alhamisi.Ili kuwa mtu wa mafanikio ni vema kutumia mbinu ya kufikiri kwa ubunifu kile unachotaka kukifanya.Ni vizuri kuwa na imani, unaweza kufanya jambo lako na likafanikiwa, kwani unapoamini litafanikiwa, akili yako itazidi kutafuta njia ya kulifanikisha zaidi.Kuamini kuwa unaweza kufanya jambo kubwa, kunafungua njia ya mafanikio. Kamwe usiseme ama kufikiri kuwa huwezi kufanya jambo fulani katika maisha yako, badala yake, jaribu kufanya kile unachofikiri kuwa huwezi.Usiruhusu mambo ya mila na desturi ama utamaduni uliouzoea kutawala akili yako.Kuwa mtu wa kupokea mambo na mawazo mapya kila wakati, kisha uyafanyie kazi.Kila wakati jaribu njia mpya katika kufanikisha mambo yako, pamoja na kuwa mfuatiliaji wa shughuli...

BUNI NJIA ZA MAFANIKIO

MSOMAJI wangu, katika mfululizo wa makala hii ya maisha yetu, nimedhamiria kukuletea kitu kipya kila Alhamisi.Leo tutaangalia ujasiri unavyomfanya mtu kubuni njia mbalimbali za mafanikio.Kila mmoja anapenda kuwa na mafanikio katika maisha yake, lakini mafanikio hayaji tu bila kufanya juhudi ama jitihada za dhati.Mojawapo ya njia inayoweza kukutoa hapo ulipo na kukupeleka katika hatua nyingine nzuri zaidi ni ubunifu.Mtu yeyote anayependa kuwa na mafanikio maishani, inambidi awe mbunifu katika nyanja mbalimbali ili kama yeye ni mfanyabiashara aweze kuteka soko kubwa.Unaweza kuwa mbunifu katika fani yoyote ile uliyonayo, ama kipaji ulichopewa na Mungu, kitakachokufanya uwe mtu tofauti katika maisha yako.Kama wewe ni mwalimu ambaye ni mbunifu wa kufundisha, maisha yako yatakuwa mazuri kwa sababu...

JINSI YA KUPANGA MALENGO YAKO

MSOMAJI wangu, nakukaribisha tena katika mfululizo wa makala hizi za maisha yetu, zinzokujia kila Alhamisi.Leo tutaangalia jinsi unavyoweza kupanga malengo makubwa katika maisha yako.Watu wengi hushindwa kufikia malengo makubwa kwa kuwa, mara zote hujikatisha tamaa kuwa hawawezi kufanya jambo kubwa la kimaendeleo, kabla ya kujaribu kulifanya.Tabia ya baadhi ya watu hao wanaokuwa na malengo madogo katika mazingira wanayoishi, ina maanisha eneo hilo hakuna ushindani wa kimaendeleo, ama wao wenyewe hawana jitihada za dhati za kupiga hatua zaidi mbele.Lakini ikimbukwe kuwa, katika kutafuta mafanikio hayo ili uwe na maisha bora, usimwangalie mtu jinsi alivyo, kwamba ana urefu gani, ana pesa kiasi gani, digrii aliyonayo ama kuangalia historia ya maisha yake, bali hupimwa kwa uwezo wa kufikiri kwake.Watu...

ONDOA HOFU, KUWA JASIRI

KARIBU msomaji wa safu hii ya maisha yetu inayokujia kila siku ya Alhamisi.Leo tutaangalia jinsi ya kuwa na ujasiri na kuondoa hofu katika maisha yako.Hofu si jambo zuri katika maisha, lakini ni ukweli usiopingika kuwa, kila mtu hupatwa na hofu kutokana na jambo fulani analokutana nalo.Hofu hiyo hukaa nayo kwa dakika chache kabla ya kutoweka. Lakini wapo wengine hukaa nayo kwa siku nzima. Kutegemea ni jinsi gani unavyoidhibiti hofu hiyo.Watu wengi hukabiliwa na hali ya wasiwasi, kutokutulia, kudharauliwa, kuchanganyikiwa au mambo yake kutokuwa katika mpangilio mzuri, pamoja na kuwa na mawazo hasi.Hali hiyo, isipodhibitiwa kwa haraka huleta usumbufu katika maisha yake. Hivyo ni vema kujijengea hali ya ujasiri na kuondoa hofu, katika jambo lolote lile unalolifanya.Kwa mfano, kama umeamua kulima...

JIAMINI UTAFANIKIWA

MSOMAJI wangu, katika mfululizo wa makala hizi za Maisha Yetu, nimedhamiria kukuletea kitu kipya kila Alhamisi.Leo tutaangalia jinsi ambavyo kila mmoja anapaswa kujijengea uwezo wa kuweza kujiamini ili kupata mafanikio.Kila mmoja anapaswa kutamani kuwa kiongozi yeye mwenyewe, ili aweze kujenga uwezo wa kuwa na maendeleo binafsi, pasipo kutamani maendeleo ya mtu mwingine.Kwasababu hakuna mtu atakayemlazimisha mtu mwingine kupata mafanikio.Lakini kwa upande mwingine, suala la mafanikio ni jambo linalotokana na muda uliopo, kujitoa na kufanyia kazi mambo mbalimbali mtu anayoyapanga.Hivyo ujue wazi hakuna mtu atakayekulazimisha wewe kupata mafanikio, bali inakupasa kufanya bidii binafsi ili ufikie matarajio ya juu uliyojipangia.Haya yakizingatiwa, kila mmoja atakuwa na ari ya kujisimamia, kufanya...

HUU NDIO UGONJWA WA KUSHINDWA KUFIKIA MALENGO

MSOMAJI wangu, katika mfululizo wa makala hizi za maisha yetu, nimedhamiria kukuletea kitu kipya kila alhamisi.Leo tutaangalia jinsi ya kukabiliana na ugonjwa wa kushindwa kufikia malengo.Kila mmoja tayari ana vifaa vya kutosha katika maabara yake ambayo anaweza kuitumia kwa ajili ya kazi na kujifunza.Maabara ambayo ina kila kitu kinachokuzunguka katika dunia hii. Ambamo hutapata vikwazo, kwa kuwa kila utakachojifunza utajiona kama wewe ni mtaalamu.Ukiweza kuitumia vizuri maabara hiyo, itakuwezesha kumaliza matatizo yako ya kifamilia kama vile, kulipia kodi ya nyumba, kulipia ada za shule na mambo mengine yanayofanana na hayo. Hivyo unaweza kuitumia maabara hiyo kwa uhuru zaidi jinsi unavyopenda.Kwa upande mwingine, unaweza kuwaza jinsi ya kuwa na malengo makubwa katika maisha, kwa kupenda...

AKILI YAKO NI KIWANDA CHA MAFANIKO

MSOMAJI wangu, katika mfululizo wa makala hizi za maisha yetu, nimedhamiria kukuletea kitu kipya kila Alhamisi. Leo tunazungumzia ili ufanikiwe unatakiwa ufanye nini.Ni ukweli usiopingika kuwa, ili ufanikiwe katika maisha yako, inakubidi ufanye jitihada ya dhati. Kwa kujiuliza ni wapi uliposhindwa, ili uweze kuongeza bidii.Vile vile, ni vema kuangalia udhaifu wako ulipo, ili uweze kurekebisha pale unapokosea katika kufikia mafanikio unayoyataka.Watu wengi hupenda kuwa na mafanikio makubwa, lakini hawaonyeshi jitihada za dhati za kuwatoa pale walipo na kuwasogeza mbele.Mara zote hukata tamaa kwa kuwaza mambo ambayo huwarudisha nyuma, hawako tayari kukubaliana na ukweli kuwa wanaweza kufanya jambo lolote ili kufikia malengo makubwa, cha msingi kinachotakiwa ni jitihada.Hivyo basi, ni vizuri...

AMINI KUWA UNAWEZA KUFANIKIWA

MSOMAJI wangu, katika mfululizo wa makala hizi za maisha yetu, nimedhamiria kukuletea kitu kipya kila Alhamisi. Leo tutaangalia jinsi ya kuwa na malengo makubwa katika maisha.Kufikiria mambo makubwa katika maisha, kunakuwezesha kuishi maisha mazuri, yenye furaha, utimilifu, kipato kizuri, marafiki na heshima.Mafanikio maana yake ni kupata mahitaji unayohitaji, kustawi katika maisha, kuwa na nyumba nzuri, kupata safari, kuwa na vitu vipya, fedha zinazotosheleza mahitaji, pamoja na kuwapa watoto wako mahitaji ya muhimu.Vile vile kwa maelezo mengine mafanikio ni kupandishwa cheo kazini kwako, kuendelea kuwa karibu na watu katika biashara zako na maisha yako kwa ujumla.Pia kwa maelezo mengine, ni kujiheshimu, kuendelea kuwa na furaha pamoja na kutosheka katika maisha, kuwa na uwezo wa kufanya...

KUWA NA MAWASILIANO MAZURI KAZINI KWAKO

MSOMAJI, katika mfululizo wa makala hizi za maisha yetu, nimedhamiria kukuletea kitu kipya kila Alhamisi. Leo tutaangalia jinsi gani unaweza kuwa na mawasiliano mazuri katika ofisi unayofanyia kazi.Ni ukweli usiopingika kuwa, wale wote wanaofanya kazi maofisini, hutumia muda mwingi zaidi wakiwa ofisini kuliko nyumbani.Hivyo ni muhimu kufurahia kazi ile unayoifanya na kuwa karibu na wale wote unaofanya nao kazi kwa muda huo, kwa sababu, wakati mwingine kazi tuzifanyazo husababisha msongo, hivyo kama unapata msaada kutoka kwa wenzako, inakusaidia kuondoa hali hiyo.Lakini kwa upande mwingine, unaweza ukajikuta kuwa bila sababu ya msingi unapata upinzani katika shughuli zako unazozifanya kutoka kwa wafanyakazi wenzako.Na kwamba, pasipo sababu ya msingi unakuta watu wanakutendea matendo yanayokuudhi,...

Friday, August 28, 2009

SAHAU MAUMIVU ULIYONAYO UPATE FURAHA

WIKI iliyopita tuliangalia jinsi ya kudhibiti hisia zetu ili tuendelee kuwa na furaha, imeonekana kuwa watu wengi wameshindwa kudhibiti hisia walizokuwa nazo na kujikuta wako katika hali ya kukata tamaa, pamoja na kuvunjika moyo. Katika mfululizo wa makala hizi za maisha yetu, nimedhamiria kukuletea kitu kipya kila Alhamisi. Leo tutaangalia jinsi inavyokupasa uyaachie mambo yanayokusumbua, ili uishi kwa furaha. Tutaangalia jinsi ya kuachana na mambo mbalimbali tunayokutana nayo katika maisha ili kuweza kupata amani na utulivu katika mioyo yetu. Kumbuka kuwa kama una tabia ya kuachana na ya maumivu na huzuni unayokabiliana nayo, utakuwa na maisha mazuri, lakini kinyume cha hapo, utaendelea kuwa mtu asiyekuwa na furaha siku zote. Na pia ufahamu kuwa, kila mmoja wetu hukabiliana na changamoto...

HALI YA KURIDHIKA INAONGEZA FURAHA

KATIKA mfululizo wa makala hizi za maisha yetu, nimedhamiria kukuletea kitu kipya, ambapo leo tutaangalia jinsi ya kudhibiti hisia zetu ili tuendelee kuwa na furaha. Watu ambao hawawezi kudhibiti hisia zao wanajikuta wako katika hali ya kukata tamaa na kuvunjika moyo. Lakini ukweli ni kwamba, inakupasa usikate tamaa mpaka kumwazia Mungu wako mambo mabaya, kutokana na wewe mwenyewe kushindwa kudhibiti hisia zako. Hivyo ni vema kuwa imara katika hisia zako, bila kujali kama unapitia hali ya milima na mabonde, ili kutimiza malengo yako uliyojiwekea, kinyume cha hapo, utaendelea kuwa mtu usiyesonga mbele kutokana na hali ambayo umeiruhusu, ilhali ungeweza kuidhibiti. Mfano mzuri ni kwa mtu aliyeelimika, kwa kuwa yuko tayari kufundishika, ambaye ni muelewa, hataabiki kwa kuonyesha kuwa...

IKUBALI HALI ULIYONAYO UPATE FURAHA

MSOMAJI, katika mfululizo wa makala hizi za maisha yetu, nimedhamiria kukuletea kitu kipya kila Alhamisi. Leo tutaangalia jinsi unavyoweza kupata furaha kwa kuikubali hali ya upungufu uliyonayo. Si rahisi kwa mtu yeyote kukubali hali ya uhitaji aliyonayo, lakini kufanya hivyo ni jambo la muhimu. Ni ukweli usiopingika kuwa, katika maeneo yote ya maisha tunayoyaishi, kanuni zake zinafanana. Na kwamba, unakuwa na furaha pale tu unapokubali hali ile ya upungufu uliyonayo, kwa kuwa hapo ndipo kwenye hitaji lako. Kama ni kweli kuwa kila mmoja wetu hajakamilika katika eneo fulani katika maisha, kwa nini basi unakuwa hauko tayari kuikubali hali hiyo? Wengi wetu tumekuwa hatuko tayari kukubali hali ya upungufu tuliyonayo, kwa kuhofia kuwa jamii inayotuzunguka itatucheka, kututenga ama kudhalilika....

TATUA TATIZO LINALOKUSUMBUA ILI UWE NA FURAHA

MSOMAJI wangu, katika mfululizo wa makala hizi za Maisha Yetu, nimedhamiria kukuletea kitu kipya kila Alhamisi. Leo tutaangalia jinsi ya kuwa na furaha katika maisha yetu ya kila siku. Hebu tuangalie mfano huu. Mwanamke mmoja alikuwa anahojiwa na mwandishi wa habari kwenye runinga na ghafla aliulizwa swali kama ‘anadhani ni watu gani siku hizi wana furaha’. Kwa taharuki bila utulivu, mwanamke yule alikurupuka na kujibu lile swali kuwa kila mtu ana matatizo mengi, akimaanisha kuwa hakuna mtu yeyote aliye na furaha. Hii inaonyesha dhahiri kuwa mwanamke yule kwa muda ule hakutarajiwa kuulizwa swali kama lile. Na aliulizwa bila kupewa nafasi ya kuwa na maandalizi. Na kwa muda huo, alikuwa ni mtu aliyejawa na mawazo. Lakini ukweli ni kwamba furaha huwa ipo tu, bila kujali kama mtu ana...

FEDHA HAZIWEZI KUKUPA FURAHA

KARIBU mpenzi msomaji katika safu hii ya Maisha Yetu, inayokujia kila Alhamisi, lengo likiwa ni kujifunza mambo mbalimbali tunayoyapitia. Leo tutaangalia mambo yanayoweza kukupa furaha katika maisha. Mara kwa mara waweza kufikiri kuwa kama ungekuwa na gari la aina fulani, nafsi yako ingeweza kufarijika. Kama ungeweza kumpata mtu mtakayeweza kuishi maisha ya ndoa katika raha na shida, ungekuwa na furaha, kama usingekuwa na hali ya msongo kutokana na ukosefu wa fedha, ungekuwa umejitosheleza. Ni kweli unaweza kuwaza mengi zaidi ya hayo kwamba kama ungeweza kufanya jambo fulani ama kuwa na magari, nyumba, dhahabu na vitu vingine vya thamani, ungeweza kuwa na furaha, lakini hicho pia siyo kipimo halisi cha kuhitimisha furaha yako. Sasa ni wapi ambako unaweza kuipata furaha, kama si kwenye...

HOFU HUSAIDIA KUEPUKA HATARI

KARIBU mpenzi msomaji katika safu ya Maisha Yetu inayokujia kila Alhamisi. Leo tutaangalia mbinu za kuwa jasiri katika uamuzi wako unaoufanya. Katika maisha yetu ya kila siku, tunaona kwamba mbinu za kuwa jasiri ni nzuri katika kukabiliana na hatari iliyo mbele yako. Lakini kwa wakati mwingine, mtu anapokuwa na hali ya hofu inamsaidia kutokana na sababu iliyopo. Ama tunaweza kusema unapokuwa na hofu, hali hiyo inakusaidia kwa kusudi maalumu. Ila kuna baadhi ya watu ambao hufikiri kuwa, si vizuri mtu kuwa na woga ama hofu. Lakini hii si kweli. Kwani hali ya hofu husaidia, ni ishara katika ubongo wako kwamba pale huenda pakawa na hatari. Zipo sababu nzuri zinazopasa kuwa na hofu, kwa kuwa hofu inayozungumza ndani yetu ni vema kuilinda mwenyewe. Kutokana na hofu unapokumbana na jambo,...

ZUNGUMZA NA MTOTO WAKO ASIPATWE NA MSONGO

KARIBUNI wapenzi wasomaji katika siku nyingine ya leo, ambayo Mwenyezi Mungu ametujalia kuiona tena. Tunakwenda kuangalia hali ya msongo inayowakabili watoto pamoja na vijana wadogo. Ni ukweli usiopingika kuwa hali ya msongo inakuwepo katika hatua zote za maisha ya binadamu. Tunaona watoto wengi wenye umri wa miaka mitano na kuendelea, wamekuwa wakiona vitu mbalimbali katika nyumba zao ambavyo hufanywa na wazazi wao. Kwa mfano, kuna familia nyingine kila mara wazazi hugombana mbele ya watoto wao. Kama wazazi tuelewe, hali hiyo huleta hofu kwa mtoto na kuona kuwa baba au mama yake anaweza kumpiga wakati wowote. Wakati mwingine unakuta mzazi anaumwa na jino, maumivu anayoyapata anayaonyesha mbele ya mtoto wake, hali hiyo humjengea hofu. Kwani kuanzia hapo, inawezekana kabisa, mtoto...

WANAWAKE HUKABILIWA NA MSONGO KATIKA MAZINGIRA TOFAUTI

KARIBU mpenzi msomaji katika siku nyingine ambayo Mwenyezi Mungu ametujalia pumzi na uhai. Leo tutaangalia hali ya msongo inayowakabili wanawake. Wanawake wengi duniani, wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi, hali inayowafanya kupatwa na hofu, wasiwasi pamoja na kutojiamini. Changamoto nyingi huwakabili wanawake hao katika maeneo yao ya kazi, nyumbani na hata katika mazingira mbalimbali wanayokuwamo. Kwa mfano, kuna msemo usemao kuwa, binadamu wote ni sawa, lakini ukifuatilia msemo huo utaona kuwa, mara nyingi baadhi ya wanaume hawataki kukubaliana na msemo huo, kwa maelezo kuwa, wanawake hawana uwezo wa kufanya kazi zile ambazo wao huzifanya kwa umakini na uhodari. Kutokana na hali hiyo, ndiyo maana katika siku hizi za leo, wanawake nao wamekuwa wakihamasishana kugombea nafasi...

MSONGO KATIKA SEHEMU ZA KAZI (4)

NAWAKARIBISHA tena katika safu hii ya Maisha Yetu yenye lengo la kukufahamisha jinsi maisha yalivyo na yanavyopaswa kuwa. Leo tunaendelea na mada yetu ya msongo katika maeneo ya kazi ili uweze kujua jinsi ya kukabiliana na hali hiyo mara unapokutana nayo. Watafiti mbalimbali wamegundua kuwa, endapo bosi katika kampuni, atakuwa na hali ya msongo wa mawazo, ofisi, kampuni au shirika hilo litakuwa na mawasiliano mabaya. Naye mwanasaikolojia mmoja anayeshughulika na masuala ya viwandani amewahi kuelezea jinsi meneja mzuri anavyopaswa kuwa. Kwa maelezo ya mwanasaikolojia huyo, meneja mzuri anapaswa kuwa mshauri mzuri kwa wafanyakazi wake, ari ya kupenda kujituma, kupenda kufanya kazi na kushirikishana mambo mbalimbali na wafanyakazi wake. Kwa maelezo ya mwanasaikolojia huyo, endapo bosi...

MSONGO KATIKA SEHEMU ZA KAZI (3)

KARIBUNI wapenzi wasomaji katika siku nyingine ambayo Mwenyezi Mungu ametujalia kuiona. Leo tutaendelea kuangalia mada kuhusu msongo katika sehemu za kazi. Wengi wetu tumekuwa tukikabiliana na hali ya msongo katika vipindi mbalimbali vya maisha, kuanzia kipindi cha utoto hadi uzee. Hali hiyo humpata mtu anayefanya kazi, mzazi katika kipindi cha kulea watoto wake na katika vipindi mbalimbali vya maisha. Ila humjia kila mmoja kwa jinsi yake. Mafanikio yetu katika maisha na thamani ya maisha, inategemea ni jinsi gani tunavyokabiliana na hali hiyo. Tunahitaji kuelewa msongo ni kitu gani na kujifunza jinsi ya kukabiliana na hali hiyo. Mtaalamu mmoja aliwahi kuelezea fani saba ambazo haziepukiki katika suala la msongo, ambazo ni fani ya ualimu, uuguzi, umeneja, ustawi wa jamii, udereva, ...

MSONGO KATIKA SEHEMU ZA KAZI

KWA mara nyingine nawakaribisha tena katika safu hii ya Maisha Yetu, inayokujia kila Alhamisi, lengo likiwa ni kuelimisha. Wiki iliyopita tulizungumzia kuhusu msongo katika maeneo ya kazi, tuliona sababu zinazosababisha mtu kupatwa na msongo katika eneo la kazi ni hofu, ongezeko la muda wa kazi, ilhali masilahi ni madogo na msisitizo wa kuongeza uzalishaji kazini wakati hakuna ongezeko la marupurupu yoyote. Leo ni mwendelezo wa makala ile na tutaangalia jinsi ya kuondoa hali hiyo, ambayo kwanza inakubidi ujijali wewe mwenyewe. Wakati msongo katika kazi yako unaingilia uwezo wako wa kufanya kazi, ni vema kujijali wewe mwenyewe, au kusimamia maisha yako mwenyewe, ni wakati wa kuchukua hatua. Wakati unapodhamiria kujali mahitaji yako, unakuwa na nguvu ya kushinda hali hiyo ya msongo....

Pages 321234 »
Twitter Facebook