Friday, December 19, 2008

FAHAMU NJIA SAHIHI YA KUKOSOA ILI MTU ASIKUCHUKIE

KARIBUNI wapenzi wasomaji katika safu hii inayokujia kila Alhamisi. Ninamshukuru kila mmoja aliyekuwa mstari wa mbele katika kufuatilia mada mbalimbali. Wapo waliotoa ushauri, pongezi, lakini pale nilipokosolewa nilikubali kwani nia ni kuelimisha.Leo tutaangalia mifano mbalimbali katika maisha yetu tunayoweza kuitumia pale tunapotaka kumkosoa mtu yeyote aliyefanya jambo kwa makusudi au kwa kutokujua bila kumfanya ajisikie vibaya.Kwa kuanza, tumuangalie mkurugenzi mmoja aliyekuwa na viwanda mbalimbali vya kutengeneza nguo. Lakini siku moja aliamua kufanya ziara ya ghafla katika kiwanda chake kimoja.Alipofika kiwandani aliwakuta baadhi ya wafanyakazi wake wakivuta sigara karibu kabisa na kibao kinachokataza uvutaji sigara sehemu hiyo.Mkurugenzi huyo akakisogelea kibao hicho na kuwaonyesha wafanyakazi...

NJIA SAHIHI YA KUSHUGHULIKA NA MALALAMIKO

WATU wengi wamejaribu kuwashawishi wengine jinsi wanavyofikiri kufanya kwa kuzungumzia zaidi kuhusu mambo yao. Waache na wengine wazungumze.Kwani wanajua zaidi kuhusu shughuli zao na matatizo kuliko unavyodhani. Kwa hiyo ni vema uendelee kuwauliza maswali ili waweze kukwambia mambo machache wanayoyajua.Watu wengi hujikuta wakiingilia kati pale ambapo hawakubaliani na mazungumzo ya mwingine. Lakini wewe usifanye hivyo. Ni hatari. Hawatakusikiliza wakati bado wana mawazo yao mengi ya kueleza.Hivyo ni vema kusikiliza kwa utulivu na kuweka kumbukumbu kile kinachozungumzwa. Kuwa mtulivu katika hilo. Watie moyo kuelezea mawazo yao yote.Je, unafikiri utaratibu huo ni mzuri? Hebu tumuangalie mfanyabiashara. Kulikuwa na mfanyabiashara moja ambaye alikuwa akitafuta soko kwa ajili ya biashara yake, kabla...

KAMA UMEKOSEA KUBALI KOSA

KARIBUNI wapenzi wasomaji katika safu hii. Tunamshukuru Mungu kwa kutufikisha tena Alhamisi ya kwanza ya Desemba. Nafikiri kupitia safu hii umepata elimu na maarifa mbalimbali. Leo, tutaangalia jinsi inavyokupasa kukubali kosa endapo utakosea.Katika maisha yetu ya kila siku, ni vema kutambua kuwa unaweza kukosea kwa kufanya jambo makusudi au kwa kutokukusudia. Hivyo basi, endapo utakosea jambo, ni vizuri kukiri kosa pasipo kubisha hiyo ndiyo njia sahihi ya kuishi katika ulimwengu huu.Iwapo umetenda kosa lolote, ukaulizwa na kukiri kukosea, ni rahisi kwa mtu anayekuuliza kuelewa kwamba umetambua kosa lako na kulijutia, hivyo hautarudia tena, tofauti kama ungekataa na kusema hujakosea.Asilimia kubwa ya watu wanapokosea hunyamaza hadi wanapoulizwa. Lakini njia nzuri, unapokosea kujitambua mara...

JARIBU KUWA JASIRI KUKIRI KOSA

KARIBUNI wapenzi wasomaji katika safu hii ya Maisha Yetu inayokujia kila Alhamisi. Safu hii imekuwa ikielimisha, ikikosoa na hata kutoa muongozo wa maisha ya kila siku.Leo katika safu hii tutaangalia jinsi unavyoweza kujiepusha usiwe na maadui katika maeneo mbalimbali uliyopo. Kuna wakati unaweza kuona umeelemewa na mawazo pasipo kukumbana na tatizo lolote, lakini mtu anapokuambia umekosea, hilo linaweza kukufanya uwe na huzuni katika moyo wako.Hivyo basi, unaweza kumueleza mtu kwamba amekosea kwa kumwangalia, kumwambia au kutumia ishara kama njia ya kumshawishi mtu akuelewe kama vile unavyoweza kuzungumza kwa maneno.Elewa kuwa utapomwambia mtu ana makosa, unafikiri utamfanya akuamini? Hapana. Hiyo si njia sahihi, kwani unaweza kulitatua tatizo hilo kwa busara, maarifa, hekima na staha. Ukitumia...

JINSI UNAVYOWEZA KUJENGA URAFIKI

KILA mmoja hapa duniani ana jukumu la kuwa kiongozi mahali popote alipo - iwe nyumbani, kazini ama shuleni - ili kuwawezesha wengine kufanya kazi kwa kufuata kanuni na sheria zilizopo.Mfano wewe ni kiongozi katika kampuni, shirika au ofisi yoyote, ni jukumu lako kuwaangalia wafanyakazi wenzako kama wanafanyakazi zao kwa kufuata sheria na taratibu za kazi zilizopo.Kama utashindwa kuwasimamia vizuri, ikatokea mmoja wao akapatwa na madhara, jukumu hilo utalibeba wewe kama kiongozi wao. Hivyo basi, kama wewe ni kiongozi katika kampuni ya uhandisi ni vyema kuhakikisha kuwa wafanyakazi unaowasimamia wanatimiza wajibu wao, kwa kuvaa kofia za kufanyia kazi wakati wote wawapo kazini.Inawezekana wakati mwingine wafanyakazi hao wakafanya mazoea na kuacha kuvaa kofia hizo au wakadharau kufuata sheria...

TAFUTA NJIA SAHIHI YA KUTATUA MIGOGORO

JINSI jamii inavyokuwa na mfumo wa aina fulani ya maisha, kuna kila uwezekano wa kujenga mizizi inayoweza kusababisha mikwaruzano mbalimbali.Ni vema kuelewa kuwa, kila jamii ina mfumo wake, hivyo wengine kuona kuwa, hawatendewi haki kama wenzao, hali ambayo itaweza kuchangia kutokuelewana au migongano.Hali hiyo ya kutokuelewana hutokea hasa pale kiongozi wa nchi, wilaya, kijiji, mtaa, kwenye maeneo ya kazi au katika shughuli yoyote inayowashirikisha watu wengi, kiongozi huyo, anaposhindwa kuwawakilisha wote kwa usawa.hali hiyo huwa hutokea kwa kiongozi yeyote ambaye hayuko makini katika utendaji wake, kwani kila mwanadamu ana mahitaji muhimu, hupenda kuwa salama na kutambulika. Sasa basi, ikiwa mahitaji yake hayafikii malengo iliyokusudia, husababisha maamuzi mabovu kutolewa, amani kutoweka...

ZAWADI SI LAZIMA IWE PESA

KARIBUNI wapenzi wasomaji katika safu hii ya Maisha Yetu kila Alhamisi. Leo tutakwenda kuangalia jinsi unavyoweza kuonyesha zawadi ya upendo kwa watu, hata kama huna fedha.Kila mtu anapenda kupendwa, yakupasa kuwa na rafiki wa karibu atakayekushirikisha katika mambo mbalimbali unayokabiliana nayo.Hivyo ni vema kuwa na rafiki mzuri na kuonyesha upendo wako kwake, kwa sababu wakati mwingine unajikuta hata familia yako inakuwa mbali nawe, hivyo kipindi hicho unakuwa unahitaji mtu wa kuongea naye.Pia ni muhimu kuwa rafiki mzuri kwa sababu unajifunza ni jinsi gani ya kukutana na watu wapya na unajifunza kutokana na makosa yako.Tafuta watu ambao unapenda wawe rafiki zako, kwa kujitambulisha, kumwacha mtu mwingine kukueleza juu ya mambo anayoyapendelea.Mwonyeshe mtu huyo kuwa unamwamini, mwache ajue...

USIIGE FANYA BIASHARA UNAYOIMUDU

HABARI wapenzi wasomaji wetu. Tunamshukuru Mungu kwa siku nyingine ya leo kutuamsha tukiwa wenye afya njema. Kama kawaida leo tutakwenda kuangalia Maisha Yetu ambayo huchapishwa kila Alhamisi.Je, wajua kuwa bahati yako ipo mikononi mwako? Na kama utafanya bidii kwa kutumia mikono yako Mungu aliyokupa ni lazima utaiona.Ninamaanisha kuwa mtu yeyote anayependa mafanikio na kuamua kupambana ili kufikia malengo yake, ni lazima atafanikiwa. Mafanikio hayo yatatokana na jitihada pamoja na bidii anayoionyesha mtu huyo.Mtu yeyote ambaye hatataka kujikwamua kutoka katika hali ya dhiki aliyonayo, atabakia kuwa maskini na tegemezi. Utajiri wa watu wale wanaofanya jitihada na hata kufanikiwa hautamsaidia mtu ambaye hapendi kujishughulisha.Kama hautapenda kujikwamua kutoka katika hali ya dhiki uliyonayo,...

KUJIAMINI KUNASTAWISHA MAISHA YAKO

UTAKUWA na tofauti gani katika maisha yako endapo utakuwa mtu wa kujiamini? Ni nini zaidi utakachokipata? Hilo ni swali ambalo sote tunaweza kujiuliza.Ni ukweli usiopingika, kwamba hali ya kujiamini inasitawisha maisha yako. Hivyo unapokuwa na afya nzuri inakufanya ufikie malengo yako kwa urahisi zaidi.Unapojiamini katika maisha yako na shughuli zako za kila siku, utaweza kuwasaidia na wengine ambao unawasiliana nao katika maeneo mbalimbali iwe ni nyumbani au kazini. Vile vile endapo unakutana na mambo ya kustaajabisha, ya kushtusha au ya mshangao huna haja ya kuogopa, kwa kuwa tayari umeshajijengea hali ya kujiamini, utaikabili hali hiyo kwa urahisi.Ni vizuri kujijengea hali ya kujiamini katika maisha yako kwani watu wote walio na hali hiyo wamekuwa na viwango vya tofauti ambavyo kila moja...

Wednesday, July 23, 2008

WAZA MAMBO MAZURI

KARIBUNI wapenzi wasomaji katika safu ya ‘Maisha Yetu’. Kwa zaidi ya mwaka sasa nimeandika mambo mbalimbali yanayohusu mafanikio, jinsi ya kuishi na watu mbalimbali, kujua tabia za watu, kujijua mwenyewe na jinsi ya kupambana na maisha katika hali yoyote.Kwa kweli safu yetu imepongezwa sana na tulipokosea tulikubali ushauri kutoka kwa wasomaji wetu. Naamini mtaendelea kutuungana mkono kwa kusoma na kuendelea kutoa ushauri wa kuboresha safu hii.Wiki iliyopita niliishia sehemu inayosema; kumbuka unapoanza kuwa na hofu ya vitu vilivyopita ni kama unajaribu kupanda mazao yako kwenye vumbi.Maana yake ni kwamba yale yaliyopita usiyasumbukie, bali ugange...

ONDOA WASIWASI KATIKA MAISHA USONGE MBELE

KARIBUNI wapenzi wasomaji wa safu hii inayowajia kwa lengo la kufundisha na kubadili maisha yetu. Pia safu hii huweza kumtoa mtu katika hali fulani aliyokuwa nayo na kumweka katika hali nyingine.Wiki iliyopita tuliishia sehemu iliyoeleza, unapokuwa kwenye wakati mgumu, kama unaweza kuiondoa hali hiyo ni vizuri, lakini kama huwezi usiipe nafasi moyoni mwako.Endapo utaipa nafasi hali hiyo, itarudisha nyuma maendeleo yako kwa kuwa kila utakapotaka kupiga hatua, hofu ya kufa au kuugua na kuacha mali zako hukujia.Katika vipindi mbalimbali mtu anavyopitia, amekuwa akikutana na hali isiyo nzuri kutokana na mzunguko wa dunia.Hivyo, unapojikuta katika...

KUBALIANA NA HALI USIYOWEZA KUIBADILI

KARIBUNI wapenzi wasomaji katika Safu ya Maisha Yetu, ambayo huelimisha, huadilisha na kubadilisha mambo mbalimbali tunayokabiliana nayo katika maisha yetu ya kila siku.Wiki iliyopita tulimwona Steven baada ya kufiwa na watoto wake wawili mfululizo aliishi kwa hofu na kukata tamaa kwa muda mrefu, lakini siku moja mtoto wake wa kiume (5) alimwomba baba yake amtengenezee boti, ambayo ilimchukua muda mrefu kuimaliza.Kwa maelezo ya Steven, kutengeneza boti hiyo kulichukua muda wa saa tatu, lakini ilipokwisha aligundua muda huo alioutumia katika kazi aliyokuwa akiifanya, uliweza kumpumzisha akili yake na kumpa amani ambayo aliipoteza kwa muda mrefu baada ya kufiwa na watoto wake.Tokea hapo, aligundua kuwa ni vizuri mtu ajishughulishe katika kipindi kigumu anachopitia kama vile kufiwa na mke, mume,...

KUJISHUGHULISHA NI NJIA YA KUONDOA HOFU, WASIWASI

NI vizuri ukakabiliana na hali ya wasiwasi inayokusumbua na kuanza siku mpya. Wasiwasi mara nyingi unasababisha uso wako kuharibika, kukunjika, kupatwa na chunusi, vipele vidogo vidogo, ngozi kukunjamana, nywele kubadilika rangi na wakati mwingine kukatika.Unaweza kuona hali hiyo kuwa ni ya kawaida, lakini sivyo unavyofikiri, hivyo unaweza kukabiliana nayo kwa kuondoa hali hiyo ya hofu na wasiwasi.Je, unapenda maisha? Je, unapenda kuishi maisha marefu na kufurahia afya bora? Unatakiwa kuwa na amani ndani ya moyo wako ambayo itakuwezesha kuishi kwa kujiamini.Tuangalie mfano wa kijana Dave, ambaye alihakikishiwa na daktari wake kuwa ana ugonjwa...

ONDOA WASIWASI ANZA MAISHA MAPYA

MWANAFUNZI aliyekuwa akichukua masomo ya udaktari, alikuwa na wasiwasi wa jinsi ya kufaulu mitihani yake ya mwisho ya kumaliza chuo. Na hata atakapomaliza masomo yake na kufaulu atapelekwa wapi kufanya kazi aliyoisomea na jinsi gani ataweza kumudu maisha.Wakati akitafakari hayo, alijikuta anasoma maneno machache ambayo yalibadilisha mtazamo wake huo, na kumfanya kuwa daktari mmoja maarufu katika kizazi chake, na hata alipofariki kurasa 1,466 ziliandikwa kwa ajili ya kueleza wasifu wake.Maneno hayo ni - “Kazi yetu si kuona kwa upeo mdogo kilicho mbali, bali ni kufanya kile tulichonacho mkononi”.Hata hivyo, mwanafunzi huyo aliamini kuwa njia inayowezekana kuandaa mambo ya kesho ni kufikiri kwa ufahamu wote, pamoja na kuwa na shauku ya kufanya kazi ya leo vizuri zaidi.Aligundua kuwa hiyo ndiyo...

Thursday, July 10, 2008

Bill Gates

Wengine kufikia mfanikio kama aliyo nayo Bill Gates, huona ni ndoto na jambo lisilowezekana, kabisa, lakini amini inawezeka...

Friday, June 27, 2008

HATA WEWE UNAWEZA KUFANIKIWA

MAFANIKIO hutokana na jitihada katika maisha tunayoyaishi. Watu wengi wanaopenda kufanikiwa mara zote hutafuta mbinu mbalimbali ili kutimiza ndoto zao. Hivyo basi unatakiwa kuota ndoto ya mafanikio yenye malengo makubwa.Binafsi ninaamini katika malengo hayo kuwa kuna mafanikio endapo utamaanisha. Wakati mtu anapoanza kuwa na malengo makubwa, anaanza kwa kufikiri jinsi Mungu alivyomwezesha katika jambo hata kufikia hatua na kufanikiwa.Ndoto hiyo ya mafanikio haina gharama, ni jinsi ya unavyoweza kujipangia muda na ratiba zako. Kumbuka ukiwa na malengo ya mafanikio haitakugharimu chochote.Unaweza ukawa na malengo ya kuanzisha mradi mkubwa pasipokuwa na fedha, inabakia kuwa ni ndoto tu. Mungu alianza kuumba dunia ikiwa haina kitu. Tunaweza kuwa na malengo makubwa ya mafanikio katika maisha yetu,...

JINSI YA KUDHIBITI HASIRA

WAKATI mwingine, hasira na kuchanganyikiwa kwetu kunasababishwa na matatizo yasiyozuilika katika maisha yetu ya kila siku.Si kila hasira haina mpangilio, na mara nyingi inatokana na mambo ya kiafya, ni hali ya asili inayojitokeza katika mambo tunayokutana nayo.Njia sahihi ya kukabiliana na tatizo linalokukabili, ambalo linakusababishia hasira, si tu kulenga katika kutafuta muafaka, lakini zaidi ni jinsi gani ya kulichukua na kukabiliana nalo.Kutatua matatizo yanayokusababishia hasira kutaleta matokeo mazuri, lakini pia si kujiadhibu mwenyewe kama jibu halitakuja kama ulivyotarajia.Watu wenye hasira mara nyingi hurukia jambo na kulifanyia maamuzi,...

KABILIANA NA CHANGAMOTO KATIKA MAISHA

KUNA wakati maisha yako yanaporomoka kutokana na kupatwa na misukosuko ya maisha kama vile kufiwa na mke, mume au mtoto wako, kusalitiwa na marafiki uliowategemea maishani mwako, kukimbiwa na mke au mume wako, kufilisika, kupoteza kazi uliyokuwa ukiitegemea, au daktari kukuambia kuwa ugonjwa unaokusumbua si rahisi kupona.Hali hiyo inapokutokea, unajikuta unakata tamaa ya maisha na kujiona kuwa hustahili kuishi katika dunia hii inayokuzunguka, lakini kumbuka hiyo ni njia ya kupitia katika maisha haya tunayoishi.Hivyo ni vizuri kumtafuta rafiki yako wa karibu au kiongozi wako wa dini kwa msaada zaidi. Kwani viongozi wa dini mara nyingi wamekuwa...

TAFUTA NJIA YA KUTATUA MATATIZO YAKO

NI jambo la kawaida kuchukua jukumu endapo kitu chochote kitakwenda vibaya, ambacho umekisababisha mwenyewe, lakini unapojenga tabia ya kujilaumu mwenyewe kwa kila jambo, unaweza kuwa na wakati mgumu katika hilo.Unapojikuta ukijilaumu eti kwa kuwa watu wengine wana furaha katika familia zao au maisha yao, wana mafanikio kutokana na kufanya kazi zao kwa bidii, hali ya mahusiano katika familia zao imeimarika wakati kwako inasuasua, jaribu kutafuta njia nyingine ya kukuondolea hali hiyo inayokutesa.Njia hizo ni pamoja na kuzungumza na familia yako, wazazi wako, watoto wako, wafanyakazi wenzako wale ambao wanaweza kukupa neno la busara, kiongozi...

Pages 321234 »
Twitter Facebook