Wednesday, April 29, 2009

BOSI WAKO ANAPOKUVUNJA MOYO USIKATE TAMAA

KWA mara nyingine tena, ninapenda kuwakaribisha wasomaji wangu katika safu hii inayokujia kila alhamisi, ili uweze kuelimika kwa kupata mawazo mbalimbali.Leo tutaenda kuangalia njia mbadala za kufanya baada ya kukumbana na misukosuko mbalimbali kutoka kwa bosi, mkuu wa kitengo au mkurugenzi wako.Watu wengi wamekuwa wakivunjika moyo na wengine wao kuamua kuacha kazi eti kwa sababu bosi wake hampendi, lakini ikumbukwe kuwa hiyo siyo suluhu kwako kwani kuna hatua mbalimbali za kufuata kabla ya kuchukua uamuzi wako ulioukusudia.Je umeshoka? Umekata tamaa? Huna furaha? au Hupati hamasa katika kazi yako? Pia inawezekana kwamba mawasiliano yako na bosi wako yanakufanya uwe mnyonge, kwa kuwa ni mwonevu, mkatili na mkandamizaji. Anaingilia faragha yako, anakudhibiti, mchokonoaji au kukuona huna maana.Lakini...

TUNAWEZAJE KUEPUKA MIGONGANO?

KARIBUNI wapenzi wasomaji katika safu hii ya Maisha Yetu. Leo tutaangalia ni jinsi unavyoweza kuepuka migongano isiyokuwa ya lazima.Ni jambo jema na la busara kuchagua nini cha kusema kuliko kusema kile unachochagua. Kwa kufanya hivyo utajiepusha na migogoro.Mara kadhaa wanandoa wamekuwa wakitengana, marafiki kufarakana na wafanyakazi kukosa ushirikiano. Je, unafahamu ni nini kinasababisha hali hii ya huzuni? Sababu kubwa kuliko zote ni kutokuwa na mawasiliano mazuri. Tumeshashuhudia watu wazuri wakitengana kwa sababu ya kutokuelewana. Walifikiri walikuwa na mawasiliano, kumbe sivyo.Tatizo ni kwamba watu wengi hawawezi kutofautisha kati ya kuzungumza na kuwasiliana, hali inayochangia migogoro. Mawasiliano yana sehemu mbili ya kuzungumza na kusikiliza. Mzizi wa neno mawasiliano maana yake ni...

Wednesday, April 8, 2009

MPE MWENZA WAKO NAFASI YA KUZUNGUMZA

KARIBU mpenzi msomaji katika safu hii inayokujia kila Alhamisi, kwa lengo ya kukufanya wewe ujue mbinu mbalimbali zitazokufanya ufanikiwe katika maisha yako.Katika maisha yako unayoishi, kamwe usiwadhalilishe wengine kwa jambo lolote lile.Nasema hivyo kwa sababu rafiki yangu aliniambia kuwa hajawahi kujisikia vibaya kama siku moja aliyoalikwa kwenye chakula cha jioni na rafiki yake.Alisema rafiki yake huyo, kila mara alikuwa akimdhalilisha mkewe alipokuwa akitaka kuchangia mada yoyote ambayo walikuwa wakiichangia.“Mke wangu hana akili kwenye kichwa chake,” alisema mtu huyo aliyekuwa ameandaa chakula kwa ajili ya rafiki zake.Baadhi ya wanaume wanafurahia kuwakosoa na kuwavunja moyo wake zao, au rafiki zao. Hali hiyo inaweza kuwafanya wakajisikia kana kwamba ni washindi kwa wakati huo, lakini...

KUWA JASIRI KATIKA MAAMUZI YAKO

KWA mara nyingine wapenzi wasomaji tunakutana katika safu hii ya maisha yetu inayokujia kila Alhamisi kwa ajili ya kukuelimisha pamoja na kukuongezea maarifa kwa namna moja ama nyingine katika kukupatia maendeleo.Leo tutaangalia jinsi ambavyo maamuzi mazuri unayoyaamua katika maisha yako yanavyokupa ujasiri wa kusonga mbele katika kufikia malengo uliyojiwekea.Kumbuka kama unataka kuwa mtu fulani katika jamii au kuwa kiongozi, ni vema ukawa jasiri wa maamuzi yatayokufikisha kwenye mafanikio.Pia wapo watu wanaokuwa thabiti katika kufanya maamuzi, lakini pia, kutekeleza inakuwa shida. “Ni jambo moja kuwa thabiti kufanya maamuzi, lakini ni jambo Jingine kutendea kazi.”Unapothubutu kufanya jambo lolote ambalo unaona kuwa baadaye litakuletea mafanikio, wewe ni jasiri. Tofauti na hapo unajimaliza...

MALENGO NI MUHIMU KATIKA MAISHA

KARIBUNI wapenzi wasomaji wa safu hii ya Maisha Yetu. Leo ni siku nyingine mpya tunayoangalia ili tufanikiwe katika maisha yatupasa kufanya mambo gani.Kama unataka kufanikiwa katika maisha yako, inakupasa uwe wazi kwa kile unachohitaji kukifanya. Kwa mfano, unaweza kumuuliza kijana mdogo anatarajia kuwa nani katika maisha yake, hapo utapata jibu kutoka kwake. Kijana huyo anaweza kukwambia, anataka kuwa mwana anga, rubani, daktari, muigizaji au askari. Watoto hueleza kwa uwazi kile wanachohitaji.Kwa upande mwingine swali hilo hilo ukimuuliza mtu mzima kile anachokitarajia katika maisha yake, mara nyingi huwa hayuko wazi kuelezea matarajio yake ni yapi. Hapa inaonyesha kuwa watu wengi wanashindwa kufikia matarajio waliyonayo kwa kuwa hawana malengo thabiti ya maisha yao.Ni nini unachokihitaji...

ZUIA HASIRA, HISIA ZINAZOKULETEA MAUMIVU

NI siku nyingine njema ambayo Mwenyezi Mungu ametujalia kuiona tena. Tunayo kila sababu ya kumshukuru kwa pumzi na uhai aliotupa.Mwanadamu yeyote aliyeumbwa na Mwenyezi Mungu ana hisia mbalimbali ambazo humfanya kuwa hivyo alivyo. Mojawapo ya hisia hizo ni hasira. Lakini ni vema kujitambua na kuitawala hasira yako kabla haijakutawala.Hivyo basi, kama hupatwi na hasira, ni lazima utakuwa na tatizo. Pia ni vema kutambua kuwa kupatwa na hasira ni hali ya kawaida. Ni suala la hisia za muhimu kwa afya yako. Tatizo linakuwepo pale mtu anaposhindwa kuzuia hasira yake na kuchukua hatua na kuanza kupigana au kugombana na watu pasipo sababu ya msingi.Hasira isiyo na mipaka inasababisha vurugu zinazoleta uharibifu. Ni sawa na ugonjwa, usipoizuia hasira inaweza kukudhuru na kukukereketa moyoni kwa njia...

ILI UFANIKIWE KAMILISHA JAMBO MOJA NDIPO UANZE LINGINE

NI siku nyingine tena ambayo Mwenyezi Mungu ametuamsha tukiwa wazima na wenye afya njema. Karibu mpenzi msomaji katika safu hii ya Maisha Yetu inayokujia kila alhamisi kwa lengo la kukuelimisha na kukuadilisha.Kumbuka, katika maisha hakuna njia ya mkato ya mafanikio. Mafanikio yoyote yana gharama kubwa. Uwezekano wa kufanikiwa upo, thawabu ipo lakini mpaka uwe na uhitaji huo. Ili ufanikiwe, yakupasa ufanye kazi kwa bidii, kwani ni muhimu kujishughulisha na kitu unachokipenda na kuongeza ujuzi wa kufanya kazi yako kwa ubora unaotakiwa.Siri nyingine ya mafanikio katika maisha ni uaminifu, kwa maneno mengine tunasema, uaminifu ni siri ya mafanikio. Kama utakuwa mwaminifu, utaaminiwa. Ina maana utakuwa mwaminifu katika shughuli zako zote unazozifanya.Hata katika maeneo ya kazi, kila mwajiri hupenda...

Pages 321234 »
Twitter Facebook