MPENZI msomaji, nakukaribisha tena katika safu hii ya Maisha Yetu. Leo tutaangalia njia mbalimbali za kukusaidia unapopatwa na matatizo.Mara nyingi mtu anapopatwa na matatizo hubabaika na kujikuta hana msaada wowote.Mtu huyo huwa anashindwa kujikubali kama yupo salama na lipo tumaini jipya baada ya matatizo hayo anayokabiliana nayo.Ni watu wachache wanaojikubali kuwa wana matatizo na kutafuta njia ya kukabiliana nayo.Wengi walio na misukosuko hukosa furaha na kujiona kuwa ni wanyonge, waliokataliwa na jamii inayowazunguka.Hali hiyo huwafanya afya zao kuzorota na kukabiliwa na magonjwa mbalimbali kama ya moyo na vidonda vya tumbo.Kutokana na hali hiyo inayomkabili mtu huyo, jamii, ndugu na hata marafiki zake huwa mbali naye na kuacha kutoa ushirikiano wa karibu kwake.Ni vizuri kuelewa kuwa,...