Na Mwandishi
Wetu
MKUU wa
Wilaya ya Bagamoyo ambaye pia ni mwanahabari, Ahmed Kipozi amesema kuwa uhuru
wa vyombo vya habari maana yake si upotoshaji wa habari.
Kipozi
ambaye pia ni mtangazaji mkongwe enzi za iliyokuwa redio Tanzania, televisheni
ya ITV pamoja na redio Uhuru, alisema hayo katika mkutano mkuu wa Watangazaji
kwa mwaka huu, ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Jijini
Dar es Salaam.
Alisema hivi
sasa sekta ya habari imekuwa, na kwamba utangazaji unabeba utaifa na uzalendo
hivyo lugha zinazotumika kwa miaka ya sasa zimebadilika tofauti na ilivyokuwa
zamani.
“Uhuru wa
habari maana yake si upotoshaji, lugha, nidhamu ya utangazaji vimebadilika. Ukumbuke
kuwa mtangazaji unapotangaza unajibeba mwenyewe pia unabeba taifa,” alisema
Kipozi.
Aliongeza
kuwa, hivi sasa watangazaji wengi wanaweza kutangaza lakini hawafikishi ujumbe
uliokusudiwa tofauti na ilivyokuwa miaka ile ya zamani.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Profesa John Nkoma alisema kuwa mabadiliko makubwa
ambayo yametokea katika karne hii ni utangazaji wa kutumia teknolojia ya
kidijiti.
Na kwamba
mfumo huo wa kidijiti umeleta mabadiliko makubwa kwenye maisha ya kila siku kwa
sasa unaweza kupata matangazo ya televisheni mahali popote kwa kutumia vifaa
mbalimbali kama vile kompyuta, simu za mkononi na kompyuta ndogo za mkononi kwa
kupitia mfumo wa intaneti.
Aliongeza kuwa
kwa kipindi c ha miaka 20 iliyopita sekta ya utangazaji imekuwa kwa kiwango cha
haraka hadi kufikia mwaka huu kuna vituo vya televisheni 28 na redio 94.
mwisho