KARIBUNI wapenzi wasomaji katika safu hii inayokujia kila Alhamisi. Ninamshukuru kila mmoja aliyekuwa mstari wa mbele katika kufuatilia mada mbalimbali. Wapo waliotoa ushauri, pongezi, lakini pale nilipokosolewa nilikubali kwani nia ni kuelimisha.Leo tutaangalia mifano mbalimbali katika maisha yetu tunayoweza kuitumia pale tunapotaka kumkosoa mtu yeyote aliyefanya jambo kwa makusudi au kwa kutokujua bila kumfanya ajisikie vibaya.Kwa kuanza, tumuangalie mkurugenzi mmoja aliyekuwa na viwanda mbalimbali vya kutengeneza nguo. Lakini siku moja aliamua kufanya ziara ya ghafla katika kiwanda chake kimoja.Alipofika kiwandani aliwakuta baadhi ya wafanyakazi wake wakivuta sigara karibu kabisa na kibao kinachokataza uvutaji sigara sehemu hiyo.Mkurugenzi huyo akakisogelea kibao hicho na kuwaonyesha wafanyakazi...