KUNA vitu mbalimbali ambavyo kiongozi au meneja anaweza kuvifanya ili kuweka mazingira ya kazi yako yawe katika hali nzuri na kujenga hali ya umoja, mshikamano na furaha miongoni mwa wafanyakazi.
Miongoni mwa vitu hivyo ni kiongozi au meneja huyo kujenga kuaminiwa na wale anaowaongoza. Kujenga uaminifu ni jambo muhimu kwa wale wote wanaomhusu katika eneo la kazi.
Kiongozi unatakiwa kuaminiwa kwa kile unachokizungumza kwamba utakifanya. Ni njia ya kuwaonyesha wafanyakazi kuwa kila unachokifanya ni kwa ukamilifu sio ubabaishaji, ni jukumu lako.
Pia kuwaonyesha wale unaowaongoza kuwa unatarajia kupata mambo kama hayo unayostahili kuwafanyia kutoka kwao.
Endapo maneno yako unayoyazungumza na tabia yako vinakwenda sambamba hapo utaaminiwa sana . Inaweza...